1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Milio ya risasi yasikika Nigeria

16 Aprili 2011

Milio ya risasi ya hapa na pale na miripuko ya mabomu imeripotiwa kutokea katika mji wa Maiduguri uliopo kaskazini-mashariki mwa Nigeria.

https://p.dw.com/p/10uej
Msururu wa wananchi wa Nigeria ukisubiri kupiga kuraPicha: DW

Taarifa hizo zimeripotiwa wakati wapiga kura wakijiandaa kupiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo hii leo, wiki moja baada ya kufanyika uchaguzi wa wabunge.

Rais Goodluck Jonathan anapewa nafasi kubwa ya kumshinda mpinzani wake mkubwa, Muhammadu Buhari, kiongozi wa zamani wa kijeshi. Zaidi ya watu milioni 73 wamejiandikisha kupiga kura katika vituo 120,000 vya kupigia kura nchini humo.

Nigeria ni taifa lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika likiwa na watu milioni 150 na taifa kubwa barani humo linalosafirisha nje mafuta. Uchaguzi wa rais miaka minne iliyopita uligubikwa na vurugu, wizi na udanganyifu.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (Alle+Deu14)
Mhariri: Sekione Kitojo