Milio ya risasi imerindima Sudan
25 Aprili 2023Matangazo
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa Jeshi la Sudan na kikosi cha msaada wa dharura - RSF walikubaliana kuweka chini silaha baada ya mazungumzo yaliyofikiwa jana usiku. Majaribio ya awali ya kusitisha mapigano kwa muda hayakuheshimiwa, lakini mara hii pande hizo mbili zimethibitisha kuwa zimekubaliana kuweka chini silaha kwa siku tatu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuwa Sudan iko kwenye ukingo wa kuangamia.Hayo ni wakati nchi za kigeni zikiendelea kuwaondoa raia wake walionaswa katika mgogoro huo.