MILAN:Waziri Mkuu wa Italia ashinda kura ya imani
1 Machi 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa Italia Romano Prodi ameshinda kura ya imani katika Baraza la Senate inayomwezesha kubakia bungeni.Kiongozi huyo bado anasubiri kura ya imani katika Bunge nchini humo.Bwana Prodi alijiuzulu wiki jana ikiwa ni miezi 9 tangu kuingia madarakani na baada ya kupoteza kura muhimu katika Baraza la Senate kuhusu sera zake mpya za kigeni.Mswada unaogharamiwa na serikali wa kuongeza muda wa kuepeleka majeshi ya Italia nchini Afghanistan vilevile kupanua shughuli za kijeshi za Marekani mjini Vicenza ulishindwa kupata idadi ya waungaji mkono waliohitajika.