MILAN : Kundi la Jihad Ulaya ladai kuhusika na miripuko ya London
7 Julai 2005Matangazo
Kundi lisilojulikana limedai kuhusika kwa kutumia jina la Al Qaeda kwa miripuko hiyo mjini London iliouwa takriban watu 12 na kujeruhi wengine zaidi ya 150.
Kundi linalojiita kuwa la siri la Al Qaeda la Jihadi Barani Ulaya limedai kuhusika na shambulio hilo katika tangazo kwenye tovuti na kuzionya Italia na Denmark kuondowa wanajeshi wao kutoka Iraq na Afghanistan.
Dai hilo halikuweza kuyakinishwa na halikuonekana katika tovuti zozote zile ambazo hutumiwa kwa kawaida na Al Qaeda.