MILAN : Kesi ya Berlusconi yaahirishwa
21 Novemba 2006Matangazo
Kesi ya Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi imeahirishwa hadi wiki ijayo muda mfupi baada ya kufunguliwa kwake leo hii mjini Milan.
Yeye pamoja na washtakiwa wenzake wengine 12 wanakabiliwa na mashtaka ya juu ya kodi na madai ya udanganyifu. Berlusconi mwenye umri wa miaka 70 anashutumiwa kwa kuhujumu kodi katika kununuwa haki miliki ya filamu nchini Marekani kulikofanywa na kampuni ya Mediaset kundi la kampuni ya televisheni linalomilikiwa na familia yake.
Iwapo watapatikana na hatia wanaweza kukabiliwa na kifungo cha miaka 4 hadi 12 gerezani.