SiasaIsrael
Umoja wa Ulaya wataka mapigano kusitishwa Gaza
27 Oktoba 2023Matangazo
Wakuu hao wa Ulaya, wamesema Umoja wa Ulaya utashirikiana na washirika katika Kanda ya Mashariki ya Kati kuwalinda raia, na kuwafikishia msaada wa chakula, maji, dawa, mafuta na makaazi, wakihakikisha kuwa msaada huo ''hauwanufaishi magaidi.''
Wakati huo huo, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linafanya kikao cha dharura kuanzia jana kujadili vita vya Israel na Hamas.
Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa Riyad Mansour alilitaka baraza hilo kutambua mateso makubwa yanayowafika Wapalestina katika vita hivyo alivyosema baadhi ya nchi wanachama umoja huo wanaviunga mkono.
Naye balozi wa Israel Gilad Erdan amejibu kuwa nchi yake haipigani vita na Wapalestina, bali "kundi la kigaidi la Hamas."