Wachunguzi wawili wa Umoja wa Mataifa wauwawa Congo
29 Machi 2017" Baada ya kufanya uchunguzi imegundulikana kuwa miili hiyo ni ile ya wachunguzi wawili wa Umoja wa Mataifa na mkalimani wao waliooneka katika mto Moyo," alisema msemaji wa serikali, Lambert Mende.
Msemaji huyo aliongezea kuwa wachunguzi wataendelea kuwatafuta wafanyakazi wengine wakicongo waliopotea pia.
Michael Sharp kutoka Marekani, na Zaida Catalan kutoka Sweden, pamoja na mkalimani wao Betu Tshintela, na dereva Isaac Kabuayi pamoja na waendesha pikipiki wawili, walipotea tangu March 12 mwaka huu wakati walipokuwa wakifanya uchunguzi mkubwa juu ya vurugu na ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na makundi ya majeshi nchini humo.
Inspekta wa polisi nchini Congo, Jenerali Charles Bisengimana, alisema kuwa miili hiyo ilionekana Jumatatu baina ya mji wa Tshimbula na Kanaga.
Baba wa Michael Sharp aliandika katika ukurusa wake wa mtandao wa kijamii, facebook kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa miili iliyooneka inawezekana sana kuwa ya mwanawe na mfanyakazi mwenzake.
"Sikuweza kusema kitu, maneno yote yalinipotea, " aliaandika.
Guterres Aomboleza
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, alisema kuwa uchunguzi utafanyika
ili kujua kitu gani kilitokea kwa wachunguzi hao wawili waliokufa. Mpaka sasa sababu ya
vifo vyao haijajulikana aliongozea kusema.
"Michael na Zaida wamepoteza maisha yao wakati walipokuwa wakitaka kufahamu sababu zinazochangia kuwepo kwa vurugu na ukosefu wa usalama nchini Kongo, ili kuleta amani kwa nchi hiyo na wananchi wake," alisema Guterres wakati wa maombolezi.
Baadhi ya sehemu nchi Kongo, hususan upande wa mashariki, wamekuwa na vurugu na ukosefu wa usalama kwa muda mrefu sana , lakini pia vurugu limekuwepo pia katika sehemu ya jimbo la Kasai kati ya Congo.
Alipoulizwa kama upoteaji wa wachunguzi na wataalamu wa Umoja wa Mataifa, nchini Congo unaweza kuathiri Umoja wa Mataifa kutuma wataalamu nchi humo, naibu msemaji wa Guterres Farhan alisema kuwa ana imani kuwa wataendelea kutuma wataalamu kufanya uchunguzi nchini humo, pale wanapohitajika. Aliongezea kusema pia kuwa bila shaka hatua hiyo itachukuliwa kwa kuzingatia na kufahamu pia hali ya usalama nchi Congo.
Mwandishi: Najma Said
Mhariri : Daniel Gakuba