1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Midrand, Afrika kusini. Bunge la Afrika laidhinisha ujumbe kwenda Zimbabwe.

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC38

Bunge la Afrika limeidhinisha hoja leo Ijumaa ya kutuma ujumbe maalum nchini Zimbabwe ili kuchunguza madai ya uendeaji kinyume haki za binadamu chini ya utawala wa rais Robert Gabriel Mugabe.

Baada ya saa mbili za majadiliano makali, hoja hiyo iliidhinishwa kwa kura 149 kwa 20 katika kikao cha chombo hicho cha bara hilo , mjini Midrand karibu na mji wa Johannesburg. Wabunge watatu wamesusia kura hiyo.

Ujumbe huo una lengo la kuchunguza madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala wa sheria pamoja na kukamatwa na kuwekwa korokoroni , kupigwa na kuuwawa kwa wanaharakati wa kisiasa na wafanyakazi wa vyombo vya habari.