Vilabu kushuka dimbani katika Ligi ya Mabingwa
2 Novemba 2015Mabingwa wa zamani Juventus, Paris St Germain, Manchester City and Zenit St Petersburg, timu pekee yenye pointi nyingi inaweza pia kufuzu ikiwa mambo yatakuwa upande wao katika michuano ya kesho na Jumatano. Washindi mara kumi wa kombe hilo Real watawaalika PSG katika Kundi A uwanjani Santiago Bernabeu, huku wote wakiwa na pointi saba. Mshindi atafuzu mradi tu Shakhtar Donetsk ambayo haina pointi itaipiku Malmo iliyo na pointi tatu katika mchuano mwingine wa kundi hilo.
Barca wanaoongoza Kundi E wanaweza kufuzu siku ya Jumatano ikiwa watapa ushindi wa nyumbani dhidi ya BATE Borisov ambayo ina pointi tatu, na ikiwa Roma iliyo na pointi mbili itashindwa kuipiku Bayer Leverkusen yenye pointi nne katika mpambano mwengine.
Kundi H la Valencia huenda likaamuliwa Jumatano. Zenit ambao wanaongoza na point tisa mbele ya Valencia na sita watafuzu ikiwa watashinda nyumbani dhidi ya Gent iliyo na point moja. Valencia itajiunga nao ikiwa itaipiku Olympiqze Lyon yenye pointi moja.
Katika Kundi D timu zote mbili huenda zikafuzu ikiwa viongozi Juventus walio na pointi saba watawashinda Borussia Moenchengaldbach ambao wana moja tu na City iliyo na sita iishinde Sevilla iliyo na pointi tatu. Katika timu nyingine za Premier League, Manchester United inaialika CSKA Moscow wote wakiwa na pointi nne nyuma ya viongozi wa Kundi B Wolfsburg ambao wana sita na watachuana na PSV Eindhoven walio na tatu.
Chelsea wako katika nafasi ya tatu katika Kundi G na pointi nne kabla ya mchuano dhidi ya Dynamo Kiev yenye pointi tano wakati viongozi Porto ambao wana saba wakipambana na Maccabi Tel Aviv walio na sifuri. Ni mchuano ambao Jose Mourinho lazima ashinde kutokana na masaibu yanayoizonga klabu hiyo.
Arsenal watacheza ugenini dhidi ya Bayern Munich katika Kundi F. Bayern na Olympiakos wana pointi sita kila mmoja na Arsenalo na Dynamo Zagreb wana tatu kila mmoja.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu