Michezo ya Olimpiki ya mjini Tokyo kufanyika mwakani
22 Julai 2020Michezo ya Olimpiki ya mjini Tokyo inaweza kufanyika tu mwaka ujao iwapo hali ya virusi vya corona itakuwa nzuri hadi wakati huo, mkuu wa kamati ya matayarisho Yoshiro Mori alikiambia kituo cha utangazaji cha NHK Jumatano.
Mori amesema haiwezekani kuendesha michezo hiyo iwapo hali itaendelea kuwa kama ilivyo, na kuongeza hafikiri iwapo hali hii itaendelea kwa mwaka mwingine.
Michezo hiyo ambayo ilikuwa kimsingi ifunguliwe siku ya Ijumaa , iliahirishwa mwezi Machi kwa miezi 12 kutokana na janga la virusi vya corona.
Mji wa Tokyo hivi karibuni umeshuhudia idadi ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 ikiongezeka tena. Mori amesema kuwa upatikanaji wa chanjo ndio itakuwa ufunguo wa kufanyika michezo hiyo mwaka 2021, na iwapo michezo hiyo itafanyika ama la itategemea iwapo binadamu wataweza kulishinda janga hilo.