''Wir schaffen das'' ni kauli aliyoitoa Kansela Merkel ikimaanisha tunaweza, lilikuwa kauli maarufu sana kwani ilisababisha Wajerumani kujiamini na kuweza kukabiliana na wakimbizi waliokuwa wakipiga hodi kuingia nchini mwao. Baada ya kauli hiyo, milango ya Ujerumani iliachwa wazi na maelfu kwa maelfu ya wakimbizi wakaanza kutiririka Ujerumani. Imetimia sasa miaka mitano.