1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumuiya ya NATO yatimiza miaka 70 tangu ulipoanzishwa.

Angela Mdungu
3 Aprili 2019

Mataifa kumi na mawili ya Ulaya yalianzisha Jumuiya ya kujihami ya NATO mwaka 1949 . Leo hii, Rais wa Marekani Donald Trump ana wasiwasi iwapo NATO itaweza kuhimili miongo mingine saba ijayo

https://p.dw.com/p/3G9JQ
Trump trifft  NATO Sekretär Stoltenberg
Picha: picture-alliance/Consolidated News Photos/R. Sachs

Kwa mujibu wa Katibu mkuu wa kwanza wa Jumuia ya NATO Lord Hastings Ismay lengo la kuanzishwa kwa jumuiya hiyo lilikuwa kutoushirikisha muungano wa zamani wa Sovieti, kuiingiza Marekani kundini na kuiweka Ujerumani chini. Hii ilikuwa ni baada ya Vita kuu ya pili ya Dunia wakati ambapo Muungano wa nchi za Sovieti wakati huo ulipokuwa ukidhibiti nusu ya Ulaya ikiwa ni pamoja na Ujerumani Mashariki.

Ujerumani ya Mashariki haikupewa nafasi kwa muda mrefu na mwaka 1955 Serikali ya Shirikisho la Ujerumani ilijiunga na NATO mwaka 1955. Kisha Mashariki, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani,(GDR) ikajiunga na ushirikiano wa kirafiki wa makubaliano ya Warsaw uliyokuwa chini ya Udhibiti wa Umoja wa nchi za Sovieti.

Sasa ni miaka 70 imepita tangu kuundwa kwa jumuiya ya NATO  na hali inafanana na ile iliyokuwepo wakati wa vita baridi,vita kwa mara nyingine. Maafisa wa Urusi walihisi kutishwa na Jumuiya ya NATO ambayo imejitanua na sasa Urusi inaimarisha majeshi yake. Hili limesababisha Jumuiya hii kutojitanua zaidi.Kwa mfano nchi za Georgia na Ukraine zimepoteza matumaini ya kujiunga na NATO kwani viongozi wa NATO wanataka kuepuka migogoro zaidi.

Pamoja na migogoro katika jumuiya hiyo, Katibu mkuu wa sasa wa NATO Jens Stoltenberg amewahi kunukuliwa akieleza jinsi tofauti zinavyoendelea kuigubika jumuiya hiyo amesema Katika historia ya  NATO kumekuwa na tofauti nyingi lakini zimeweza kutatuliwa na kwamba wanachama wote na washirika wa NATO wanafahamu kwamba Amerika ya kaskazini na Ulaya ziko salama zaidi zikiwa pamoja.

NATO Jens Stoltenberg PK zum Ministertreffen in Brüssel
Katibu mkuu wa sasa wa NATO Jens StoltenbergPicha: picture-alliance/AA/D. Aydemir

Stoltenberg aliwahi kunukuliwa katika hotuba ya mwaka 2018 akisema haijaandikwa kwenye jiwe kuwa Jumuiya hiyo itadumu milele,na kwamba tofauti kati ya wanachama zipo.

Katika historia yake ya miaka 70, NATO imewahi kupitia kile kinachojulikana kama hali ambayo masharti ya muungano yaliwalazimu wanachama wote kutetea mwanachama aliyepigwa: na hii ilitokea katika shambulio la kigaidi lililotokea Septemba 11 mwaka 2001nchini Marekani. Hata hivyo uamuzi huu ulileta mgogoro ambao umekuwa ukistawi kwenye jumuiya hiyo.

Katika mkutano wa mwaka 2014 wa Jumuiya hiyo viongozi walikubaliana kutenga sehemu ya mapato ya nchi zao na kuyaingiza katika bajeti ya Ulinzi katika umoja huo. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameahidi kutoa asilimia 1.5 ya bajeti ya ulinzi wa jumuia hiyo mpango ambao unapingwa na chama cha SPD.

Mwandishi: Hasselbach, Christoph

Tafsiri: Angela Mdungu

Mhariri: Yusuf Saumu