1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 60 tangu madege ya kivita ya Marekani kutupa bomu la atomiki huko Nagasaki-Japan

9 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEme

Nagasaki:

Watu wasiopungua elfu sita wamekusanyika Nagasaki,kuwakumbuka wahanga wa mashambulio ya mabomu ya atomiki ya marekani miaka 60 iliyopita katika mji huo wa Japan.Milio ya honi na kengele imehanikiza tangu saa tano na dakika mbili kwa saa za Japan ,wakati ule ule wa agosti 9 mwaka 1945,madege ya kivita ya Marekani yalipoporomosha mabomu ya kinuklea katika mji huo.Watu wasiopungua 74 elfu wameuwawa.Diwani wa Nagasaki ICCHO ITOH ameyatolea mwito madola makuu yenye kumiliki silaha za kinuklea,yateketeze silaha hizo.Ameikosoa zaidi Marekani kwa kutengeneza kile kijulikanacho kama „vijibomu vya kinuklea.“

Siku tatu kabla ya Nagasaki,jeshi la wanaanga la Marekani lilitupa pia bomu la kinuklea katika mji wa Japan wa Hiroshima.