1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Operesheni Linda Nchi" Somalia

9 Desemba 2013

Taifa la Kenya linatimiza miaka 50 ya uhuru wake likiwa linakabiliwa na changamoto za kiusalama ndani na nje ya mipaka yake, lakini imeendelea kusimama kama taifa imara katika eneo la Afrika ya Mashariki.

https://p.dw.com/p/1AVY8
Wanajeshi wa Kenya nchini Somalia katika Operesheni Linda Nchi.
Wanajeshi wa Kenya nchini Somalia katika Operesheni Linda Nchi.Picha: dapd

Mnamo mwezi Oktoba 2011, Kenya ilituma wanajeshi wake nchini Somalia kukabiliana na wapiganaji wa al-Shabaab kupitia kile ilichokiita "Operesheni Linda Nchi". Katika kipindi hiki cha Kinagaubaga, Mohammed Khelef anazungumza na msemaji wa operesheni hiyo, Cyrus Oguna, juu ya umuhimu wa hatua hiyo ya Kenya kama kielelezo cha kusimama imara kijeshi nusu karne baada ya uhuru wake.

Kusikiliza mahojiano haya, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mahojiano: Mohammed Khelef/Cyrus Oguna
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman