1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 50 ya mapinduzi ya Cuba.

Sekione Kitojo30 Desemba 2008

Cuba inatimiza miaka 50 tangu pale vijana wa kimapinduzi wakiongozwa na Fidel Castro walipoingia nchini Cuba na kupambana na utawala wa dikteta Batista.

https://p.dw.com/p/GPR3
Rais wa Cuba, Raul Castro , kushoto, akiwa pamoja na rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil wakati akiwasili katika mkutano wa mataifa ya America ya kusini mjini Brasilia.Picha: AP

Mparaganyiko wa mfumo wa kisiasa, marais ambao wamekuwapo na kuondoka, vita na mashambulio, ushirika uliovunjika, ujenzi mpya wa nchi,... miaka 50 ya historia imejitokeza katika eneo la Amerika ya kusini. Pamoja na hayo Cuba na utamaduni wake wa kimapinduzi imeendelea kudumu mbali na yote hayo, ikikumbatia mwendelezo wake wa nadharia ya Kisoshalist ikikabiliana na mabadiliko ya kihistoria.


Hakuna kitu ambacho kimeendelea kusalia kama kilivyokuwa siku ya Januari mosi, 1959, wakati wapiganaji wakiongozwa na kijana, mwenye ndevu nyingi Fidel Castro walipoingia kishujaa katika mji wa kusini mashariki wa Santiago de Cuba , wakitangaza ushindi wa mapinduzi ambayo hayakuwa bado ya kisoshalist na ambayo baadaye yalipata pigo la kimataifa kwa kiasi kikubwa kwa nchi ndogo kama ya kisiwa hicho katika eneo la Caribiki.

Usiku siku moja iliyopita , dikteta Fulgencio Batista alikuwa amekwisha kimbilia Marekani, akiacha kisiwa hicho mikononi mwa waasi. Wanamapindizi vijana walikuwa wanapanga kuujenga upya mfumo mzima, lakini wachache waliweza kufikiria kuwa kazi yao bado ingekuwa inaendelea kuonekana hadi leo, hata kama ni katika hali ya kulega lega, miaka 50 baadaye.

Ushindi kamili ulikuja kiasi siku nane baadaye, Fidel Castro alipoingia mji mkuu Havana, akivalia nguo za kijani za kijeshi ambazo zilikuwa maarufu miongoni mwa wanamapinduzi.

Mdogo wake Raul , mtu mwingine ambaye anahusishwa na mapinduzi ya Cuba , alikosa picha ya ushindi ya pamoja kwasababu alibaki mjini Santiago de Cuba.

Pamoja pia na Ernesto Che Guevara, mzaliwa wa Argentina , ambaye amekuwa kielelezo cha uasi hali ambayo inaishi kwa dhana hadi hii leo kama hadithi za kale.

Wengine wamo katika picha hiyo ya pamoja ya ushindi , kama Huber Matos, lakini historia ya kimapainduzi iliwafuta baadaye kutoka katika safu kwasababu hawakuweza kustahili njozi ya usoshalist ambao ulikuwa unajipatia umaarufu.

Wengi kama Matos, ambaye alitumikia miaka 20 jela nchini Cuba kabla ya kwenda kuishi uhamishoni , anasisitiza kuwa usoshalist haukuwa mpango wao wakati walipochukua silaha mwaka 1956, wakati wapiganaji 82 wakiongozwa na Fidel Castro walipowasili nchini Cuba wakitokea nchini Mexico katika boti iliyokuwa ikiitwa Granma kwa azma ya kupambana na utawala wa Batista.

Sifa bainifu ya usoshalist , ya mapinduzi hayo ilitangazwa rasmi miaka miwili baada ya ushindi, na baada ya mashambulizi kadha ambayo Cuba iliielekezea kidole Marekani hapo Aprili 16, 1961.

Castro alisema kuwa haya ni mapinduzi ya kisoshalist na kidemokrasia ya kinyonge, yaliyofanywa na wanyonge, na kwa ajili ya wanyonge. Hiyo iliondoa wasi wasi kuhusiana na ukaribu wake na iliyokuwa Urusi ya zamani, ambayo ilikuwa inatafuta kujikita katika eneo la mataifa ya magharibi.

Siku moja baadaye , Aprili 17, 1961, Cuba mpya ya kimapinduzi ilikuwa inajitayarisha kwa ushindi wake wa kwanza dhidi ya himaya, neno lililotumika kuielezea Marekani. Katika muda wa saa 72, kisiwa hicho kilifanikiwa kuzuwia kuwasili katika eneo la Playa Giron , au ghuba ya nguruwe kwa wanaharakati 1,500 waliotayarishwa wanaompinga Castro wakisaidiwa na shirika la ujasusi la Marekani CIA, wengi wao walikamatwa. Uhusiano mbaya na Marekani ulikuwa umetiwa chapa wakati huo daima, ama kwa kiasi fulani miongo kadha baada ya hapo.



►◄