1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 50 tangu Ujerumani ijiunge na Umoja wa kujihami wa Magharibi-NATO

5 Mei 2005

Ilikua tarehe 6 Mei 1955.

https://p.dw.com/p/CHgv
Bendera ya Umoja wa NATO
Bendera ya Umoja wa NATO

Hatua hiyo ilikuwa muhimu sana katika ulinzi wa nchi hiyo iliyokuwa katika mstari wa mbele kwenye mpaka wa mvutano baina ya nchi za Ulaya ya mashariki na magharibi.

Kuundwa kwa mfungamano wa kijeshi NATO, kulikuwa tukio muhimu sana kwa usalama wa Ujerumani magharibi.

Ujerumani magharibi iliingizwa katika mtandao wa ulinzi wa nchi za magharibi.

Umuhimu wa hatua hiyo unatokana na kutambua kwamba sehemu nyingine ya Ujerumani ambayo wakati huo ilikuwa inaitwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani ilikuwa katika mfungamano wa kijeshi wa nchi za kikomunisti za mkataba wa Warsaw ,chini ya uongozi wa Urusi.

Hadi tarehe hiyo sita mei mwaka 1955 Ujerumani magharibi haikuwa na jeshi lake.

Lakini hatua kwa hatua Ujerumani ilianza kuunda jeshi . Lakini Ufaransa ilikuwa na wasi wasi juu ya Ujerumani kuanza kujijenga upya kijeshi.

Mvutano katika eneo la Ujerumani ulishtadi zaidi baada ya Ujerumani mashariki, kujiunga na mfungamano wa kijeshi wa nchi za Ulaya ya mashariki , Warsaw Pact chini ya uongozi wa Urusi.

Rais wa Ujerumani bwana Horst Köhler

amesema kwamba hatua ja Ujerumani kujiunga na NATO ilikuwa muhimu sana kwa usalama na uhuru wake.

Ujerumani ilikuwa mpaka baina ya nchi za mashariki na magharibi,mfungamano wa NATO ulikuwa unatazamana ana kwa ana na nchi za mkataba wa Warsaw.

Nchi wanachama na hasa Marekani tokea siku ya kwanza ziliipa Ujerumani uhakika wa kuishi katika uhuru na amani. Nchi hizo zililisimama kidete katika kuhakikisha usalama wa Ujerumani.

Baada ya kuondoshwa kwa kuta la Berlin sehemu nyingine ya Ujerumani, yaani Ujerumani mashariki pia imekuwa sehemu ya Nato.

Kutokana na mabadiliko hayo ya kisiasa,majukumu ya Ujerumani duniani pia yamebadilika. Sasa Ujerumani inashiriki katika majukumu ya jumuiya za kimataifa kama Umoja wa Mataifa.

Kwa sasa wanajeshi alfu 5000 wa Ujerumani wapo katika sehemu mbali mbali za dunia kulinda amani kwa niaba ya Umoja wa mataifa. Baadhi ya wanajeshi hao wapo nchini Afghanistan na Kosovo.

Ujerumani imepitia katika njia ndefu hadi kufikia hali ya kuwa mlinda amani hata nje ya jumuiya ya Nato. Sasa Ujerumani ina askari wengi wa kulinda amani nchini Afghanistan kuliko nchi nyingine yoyote yaNATO.“

Hatahivyo jumuiya ya NATO sasa imebadilika kutokana na mabadiliko ya siasa duniani. Sasa jumuiya hiyo ni baraza la mashaurino juu ya masuala ya usalama na kisiasa.

Ujerumani itaendelea kuwa sehemu thabiti ya jumuiya ya NATO kwani kujiunga kwake katika jumuiya hiyo miaka 50 iliyopita kulikuwa hatua muhimu ya kuanza kurejea katika jumuiya ya mataifa ya kiungwana.