Sheria na HakiRwanda
Miaka 27 jela kwa kuhusika na mauaji ya kimbari Rwanda
31 Oktoba 2024Matangazo
Hukumu hiyo ilitolewa jana kwa Rwamucyo, mwenye umri wa miaka 65, baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika mauaji ya kimbari na kushiriki katika uhalifu dhidi ya ubinadamu .
Upande wa mashtaka umesema kuwa Rwamucyo pia alishtakiwa kwa kueneza propaganda dhidi ya Watutsi na kusimamia shughuli za kuwazika wahanga katika makaburi ya halaiki.
Rwamucyo amesema jukumu lake katika mazishi hayo ya watu wengi lilitokana na motisha ya kudumisha usafi na kukanusha kwamba manusura walizikwa wakiwa hai.
Aliondolewa mashtaka ya mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Katika kesi hiyo yote iliyodumu kwa mwezi mmoja, Rwamucyo amekanusha kufanya makosa yoyote.