Miaka 25 ya mahakama ya uhalifu kwajili ya Rwanda
7 Novemba 2019((Lakini baadaye iliundwa mahakama ya kimataifa ya kuwahukumu wahalifu walioshiriki katika mauaji hayo nchini Rwanda. Inawezekana mahakama hii ya uhalifu ikarejeshwa tena baada ya kufungwa? Jibu ni la mkanganyiko.
Ruanda mwaka 1994, redio ya wenye misimamo mikali ya kisiasa wanatoa wito wa mauaji, na Wahutu wenye misimamo mikali wanawauwa bila huruma raia wa jamii ya wachache ya Watutsi pamoja na Wahutu wenye msimamo wa kati, na miili yao ikatupwa mtoni. Katika muda wa chini ya siku 100 kwa makadirio ya Umoja wa mataifa kiasi ya watu 800,000 na milioni moja walisakwa na kuuwawa. Dunia ikiwa inatazama tu. katika uhalifu huu , ambao ni mbaya kabisa katika historia ya binadamu , jamii ya kimataifa ilitaka kutoa onyo. Kwamba hatimaye inataka kujadili na kuthibitisha kwamba sheria za kimataifa dhidi ya uhalifu sio maneno matupu , badala yake inawezekana.
Siku 100 nyingine baadaye , tarehe 8 Novemba mwaka 1994, baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha mahakama ya muda kwa ajili ya kuwahukumu wahalifu. Mwanzoni mwa mwaka 1995 mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa ajili ya Rwanda ICTR ilianza kazi katika mji wa kaskazini mwa Tanzania wa Arusha. Pamoja na kufanyakazi kwa kile kinachojulikana kama mahakama za kienyeji za Gachacha, wahusika wakuu walipelekwa mjini Arusha kuwajibishwa. Ni jaribio la sheria na mahakama ya kimataifa.
Mahakama yafika mwisho
Baada ya miaka 21 mahakama ya kimataifa ya ICTR ilifikisha mwisho shughuli zake mwanzoni mwa mwaka 2016. Boubacar Diallo hadi hii leo akiwa mwendesha mashitaka mkuu wa ICTR , alikuwa akipata shida kutoa tathimini chanya: "Kwa kiasi kikubwa tumefanyia kazi masuala mengi" anasema katika mahojiano na DW. mahakama ya rwanda iliwafikisha mahakamani , wakuu wa jeshi, wanasiasa , waandishi habari na pia wakuu wa serikali , ambao walihusika katika mauaji ya kimbari. Zaidi ya hayo mahakama ya ICTR imetayarisha sehemu kubwa ya sheria zake , ambazo leo zinatumika kama mifano katika mahakama nyingine duniani kote. " Mahakama hii inaweza kwa hiyo kuwa muhimu katika mapambano dhidi ya ukosefu wa kupatikana haki katika dunia yetu", amesema Diallo.
Mwaka 1998 mahakama ya rwanda kama mahakama ya kwanza ya kimataifa ilitoa hukumu mhalifu wa kwanza kutokana na mauaji ya kimbari. Karibu nne ya tano ya wahalifu waliohusika na mauaji hayo ya kimbari mwaka 1994 katika mwaka uliofuata walikamatwa na kufikishwa mahakamani. Mahakama ya ICTR iliwafikisha mbele ya sheria washitakiwa 93. 61 walipatikana na makosa , 14 waliachiliwa huru. Wengi wa wachunguzi wanakubaliana , kwamba kwa kiasi kikubwa na kwa jumla mahakama ya ICTR imetimiza wajibu wake.
Geraldine Mattioli-Zeltner kutoka shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights watch anathibitisha kuwa , ICTR imekuwa ni sehemu kubwa ya ujenzi wa taasisi ya kimataifa ya kufuatilia wahalifu dhidi ya ubinadamu. Mahakama ya uhalifu ya Rwanda ni jiwe la msingi ka a ujenzi wa mahakama ya kimataifa mjini The Hague. Washitakiwa wapya hawatapelekwa tena mjini ARUSHA.