1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 10 ya Uhuru wa Hong Kong

Tuma Dandi29 Juni 2007

Rais wa China Bwana Hu Jintao amewasili Hong Kong katika katika sherehe za maadhimisho ya kutimiza miaka kumi baada ya kupata uhuru wake kutoka kwa Uingereza na kurudi kuwa mamlaka ya China.

https://p.dw.com/p/CHBt
Rais wa China Hu Jintao.
Rais wa China Hu Jintao.Picha: dpa - Bildfunk

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Jintao kufanya ziara katika eneo hilo tangu alipopata wadhifa huo wa kuwa kiongozi wa nchi maarufu duniani.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kushuka katika uwanja wa ndege wa Hong Kong, Rais Jintao amesema ana kila sababu ya kufurahia maendeleo ya Hong Kong katika kipindi cha miaka kumi baada ya kuwa huru.

Rais Hu Jintao amesema anaona fahari sana kwa kuwa sasa ana matumaini kwamba wakazi wa eneo hilo wanaisha maisha mazuri na yenye maana, baada ya miongo kadhaa za kuwa chini ya utawala wa kikoloni.

Maadhimisho kamili yanafanyika hapo tarehe mosi mwezi Julai ambapo jumuiya ya kimataifa inaandika historia mpya ya Hong Kong kutokana na maendeleo yaliyofikiwa.

Watafiti wa kimataifa katika masuala ya kimahusiano wamesema mifumo miwili katika nchi moja imefanikiwa kwa kiasa kikubwa kuiendeleza Hongo Kong baada ya kipindi kirefu cha kukaliwa na wageni.

Wataalamu wa masuala ya uchumi na jamii wamesema Hongo Kong imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika maamuzi ya kidemokrasia, nyanja ya habari na mawasiliano na hivi sasa ni fahari kubwa kwa China.

Uchumi wa Hongo Kong umeonekana kuwa imara katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, hata kuushangaza ulimwengu, tofauti na jinsi wadau wa sekta hiyo walivyofikiria hapo kabla.

Pamoja na kufikia mafanikio hayo, katika kipindi cha mwaka 1997, Hong Kong ilikumbwa na fadhaa katika masuala ya pesa pamoja na shambulizi la ugonjwa wa mafua uliojulikana kwa jina la SARS kwa kitaalamu mwaka 2003 na ambao ulisababisha kupungvua kwa idadi ya watalii. Rais Huu amewapongeza maafisa kwa kupambana na ugonjwa huo unaoasababisha matatizo ya kupumua.

Wadadizi wanasema Hong kong ni mfano mzuri wa kuigwa panapohusika na nchi moja kuwa na mifumo miwili tafauti ya kiuchumi. China bara kimsingi bado ni taifa la kikoministi , wakati Hong Kong ina mfumo wa uchumi unaotegemea masoko bila ya kuingiliwa na dola.