1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mhanga wa ubakaji asamehewa Saudi Arabia

17 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CcrJ

Mfalme wa Saudi Arabia Abdullah bin Abdul-Aziz, amemsamehe mhanga wa ubakaji mwanamke aliyehukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani na viboko 200.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 19 alibakwa na genge la wanaume mwaka jana lakini akahukumiwa pamoja na wabakaji waliomhujumu kwa sababu alikuwa peke yake na mwanamume mmoja ambaye hawakuhusiani.

Waziri wa sheria wa Saudi Arabia amesema uamuzi wa mfamle Abdullah hauna maana kwamba anatilia shaka kazi inayofanywa na mahakimu nchini humo, ila ameupitisha kwa kuyajali masilahi ya umma.

Kesi hiyo ilizusha hisia mbalimbali katika ngazi ya kimataifa kuhusu kuwashughulikia wanawake kwa mujibu wa sheria ya kiislamu nchini Saudi Arabia.

Wakati haya yakiarifiwa waumini wa dini ya kiislamu wameanza hija huko Mecca hii leo. Takriban waislaumu milioni mbili wameanza safari kutoka Mecca kufuata njia aliyoifuata mtume Mohammed miaka zaidi ya 1,400 iliyopita.