1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo mkubwa wa sekta ya uchukuzi waitikisa Ujerumani

27 Machi 2023

Ujerumani imeshuhudia mgomo mkubwa katika sekta ya uchukuzi kuwahi kushuhudiwa kwa muongo mmoja na hivyo kusababisha usumbufu kwa mamilioni ya wasafiri ambao wamelazimika kutafuta njia mbadala ya usafiri.

https://p.dw.com/p/4PIE9
Deutschland Bundesweiter Streik im Verkehr hat begonnen | Bonn HBF
Picha: Jana Rodenbusch/REUTERS

Safari za ndege, treni na hata mabasi zimeguswa na mgomo huo utakaodumu kwa saa 24 kuanzia leo, ambapo wafanyakazi wanadai nyongeza ya asilimia 10.5 ya mshahara.

Uchumi wa Ujerumani ambao ni mkubwa zaidi barani Ulaya unakumbwa na misukosuko kutokana na mfumuko wa bei. Mazungumzo ya siku tatu yamepangwa kufanyika kati ya serikali na vyama vya wafanyakazi.

Waziri wa mambo ya ndani Nancy Faeser, ambaye anawakilisha serikali ya shirikisho amesema watashiriki kunako majadiliano hayo wakiwa na msimamo thabiti, wa haki na wa kujenga.