1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mgombea wa urais Uturuki ajitoa kwenye kinyang´anyiro

12 Mei 2023

Mgombea mmoja wa kiti cha uraisi katika uchaguzi mkuu unaokuja nchini Uturuki ametangaza kujiondoa kwenye kinyangányiro hicho, uamuzi unaoweza kumnufaisha mpinzani mkuu wa rais wa Recep Tayyip Erdogan

https://p.dw.com/p/4RFi0
Türkei Muharrem Ince  Wahlkampf
Picha: AFP

Mgombea huyo Muharrem Ince ni kiongozi wa chama cha siasa za wastani za mrengo cha mrengo wa shoto kiitwacho Homeland Party na alikuwa mmoja wa wagombea wakuu wanne wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa Uturukiutakaofanyika Jumapili. Ince amekuwa akikabiliwa na ukosoaji kwamba kampeni yake ingeweza kuugawa ushawishi wa upinzani unaongozwa na mwanasiasa Kemal Kilicdaroglu  anayetajwa kuwa uwezo wa kumshinda rais Erdogan. Kura za maoni ya umma zinamweka mbele Kilicdaroglu kwa alama chache.  Erdogan ambaye ameiongoza Uturuki kama waziri mkuu na baadaye rais tangu mwaka 2003, anakabiliwa na uchaguzi mgumu katika historia ya utawala wake wa karibu miaka 20.