1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgombea wa upinzani Yamandu Orsi ashinda urais Uruguay

Josephat Charo
25 Novemba 2024

Matokeo rasmi yanaonesha Yamandu Orsi, ameshinda asilimia 49.81 ya kura iklinganishwa na Alvaro Delgado ambaye amejikingia asilimia 45.90 ya kura.

https://p.dw.com/p/4nNox
Kiongozi wa upinzani Yamandu Orsi ameshinda urais wa Uruguay
Kiongozi wa upinzani Yamandu Orsi ameshinda urais wa UruguayPicha: Mariana Greif/REUTERS

Rais mhafidhina wa Uruguay Luis Lacalle Pou amempigiaa simu na kumpongeza mgombea wa upinzani Yamandu Orsi kama rais mteule wa nchi hiyo ya Amerika Kusini na kumsaidia kuanza mchakato wa kukabidhi madaraka.

Lacalle Pou ameandika katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa X baada ya kura za maoni baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa kuonyesha kwamba Orsi angemshinda mgombea wa muungano unaotawala Alvaro Delgado, lakini kabla matokeo rasmi kutangazwa.

Delgado amekubali kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliyofanyika jana Jumapili.