1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRomania

Mgombea wa mrengo wa kulia aongoza uchaguzi wa Romania

25 Novemba 2024

Mgombea wa mrengo wa kulia anayeiunga mkono Urusi Calin Georgescu, anaongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Romania.

https://p.dw.com/p/4nPe6
Calin Georgescu
Mgombea wa mrengo wa kulia anayeiunga mkono Urusi nchini Romania, Calin Georgescu. Picha: Alexandru Dobre/AP Photo/picture alliance

Wakati zaidi ya asilimia 99 ya kura zikiwa tayari zimehesabiwa, Georgescu anaongoza kwa kupata asilimia 23 ya kura akifuatiwa na mgombea wa mrengo wa kati kulia Elena Lasconi huku Waziri Mkuu Marcel Ciolacu, aliyekuwa akipigiwa upatu kushinda, akishikilia nafasi ya tatu.

Hesabu ya hivi karibuni inaonyesha kuwa Lasconi amempiku Waziri Mkuu Cialocu kwa takriban kura 2,000 na hivyo atapambana na Georgescu katika duru ya pili ya uchaguzi mnamo Disemba 8.

Hatua ya Georgescu, ambaye hana chama na alifanya kampeni kwa kutumia zaidi mtandao wa kijamii wa TikTok, kuongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo imekuja kama mshangao.