1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgombea chama cha SPD Steinbrueck ateua kikosi cha kampeni

16 Mei 2013

Kiongozi wa chama cha upinzani Ujerumani SPD Steinbrueck (13.05.2013)amejaribu kuiweka sawa kampeni yake inayoyumba katika mkakati wa kupambana na kansela Angela Merkel katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

https://p.dw.com/p/18X1Y
Peer Steinbrueck, top candidate of the German Social Democratic Party (SPD) receives standing ovations after his speech during the extraordinary party meeting of the SPD in Augsburg, April 14, 2013. REUTERS/Kai Pfaffenbach (GERMANY - Tags: POLITICS)
Peer Steinbrück akihutubia katika mkutano wa SPDPicha: Reuters

Mawaziri watatu kivuli wa chama cha upinzani cha Social Democratic SPD waliomo katika kikosi hicho watashikilia nyadhifa katika masuala ya ndani na sheria, sera za internet na kazi pamoja na masuala ya kijamii.

Lakini wajumbe wengi wa kundi hilo hata hivyo bado hawajatajwa hadharani. Wajumbe hao watatu waliotajwa leo walithibitishwa baada ya majina yao kuvuja katika vyombo vya habari na kulazimisha kutangazwa rasmi siku moja kabla ya siku rasmi ya kufanya hivyo.

Sigmar Gabriel, SPD-Vorsitzender, spricht am 09.12.2012 beim außerordentlichen Bundesparteitag der SPD in der Messehalle 8 in Hannover (Niedersachsen). Foto: Michael Kappeler/dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++
Mwenyekiti wa chama cha SPD Sigmar GabrielPicha: picture alliance / dpa

Uchunguzi wa maoni

Zaidi ya hayo , uchunguzi wa maoni ya wapiga kura unaonesha kuwa Merkel bado yuko mbele ya Steinbrueck , wakati wapiga kura walipoulizwa kuwa nani wanampendelea kuiongoza nchi yao.

Hii inafuatia kile Wajerumani wengi wanakiona kuwa ni uwezo wa kansela Merkel kulishughulikia suala la muda mrefu la mzozo wa madeni katika mataifa yanayotumia sarafu ya euro.

Jukwaa analotumia Steinbrueck katika uchaguzi huu, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa mshahara wa kima cha chini na kuwatoza kodi watu wenye kipato cha juu, linaonekana kutofanya chochote kupindua majaaliwa ya chama cha SPD katika uchaguzi huu.

SPD na maoni ya wapiga kura

Chama kinaendelea kubakia katika kiwango cha asilimia 24 ya kura kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni ya wapiga kura.

Lakini serikali za Ujerumani zinaundwa kwa kuungwa mkono chama katika uchaguzi badala ya kura ya taifa kumchagua kiongozi.

Uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni unaonesha kuwa chama cha kansela Angela Merkel cha Christian Democratic kina nafasi ya kuibuka na asilimia 40 ya kura, ambazo zitakifanya kuwa ni kundi kubwa katika bunge, katika uchaguzi wa hapo Septemba.

ARCHIV - Ein Verkehrschild zur Geschwindigkeitsbegrenzung auf 120 km/h steht am 29.04.2013 an der Autobahn A71 zwischen dem Autobahnkreuz Südharz (A 38) in Sachsen-Anhalt und der Anschlußstelle Heldrungen in Thüringen. SPD-Chef Sigmar Gabriel fordert die Einführung von Tempo 120 auf Autobahnen. «Der Rest der Welt macht es ja längst so», sagte Gabriel der in Düsseldorf erscheinenden «Rheinischen Post» (Mittwoch). Foto: Jens Schlueter +++(c) dpa - Bildfunk+++
Sigmar Gabriel anataka mwendo kasi upunguzwe hadi 120 km/hPicha: picture-alliance/dpa

Hata hivyo , uchunguzi pia unaelekeza kwa chama mshirika wa chama cha CDU katika serikali ya mseto chama kinachopendelea wafanyabiashara cha Free Democrats kuwa huenda kisiweze kupata kura za kutosha kurejea bungeni.

Hali hii itakiacha chama cha CDU kusaka mshirika mpya katika serikali, ambaye huenda ikawa ni pamoja na kile kinachojulikana kama ," muungano mkubwa " na chama cha SPD.

SPD wajikwaa

Pamoja na hayo, kampeni ya Steinbrueck kumuondoa madarakani Merkel kama kiongozi wa nchi yenye uchumi mkubwa kabisa hapa Ulaya imekumbwa na mikwamo kadha tangu alipoteuliwa kuwa mshika bendera ya chama cha SPD katika uchaguzi ujao, Oktoba mwaka jana.

Der parlamentarische Geschäftsführer der SPD-Bundestagsfraktion, Thomas Oppermann, spricht am Mittwoch (23.02.2011) im Deutschen Bundestag in Berlin. Zuvor hatte Bundesverteidigungsminister zu Guttenberg (CSU) Stellung zu den gegen ihn erhobenen Plagiatsvorwürfen Stellung genommen. Der Politiker, der wegen Plagiatsvorwürfe im Rahmen seiner Doktorarbeit, in die Schlagzeilen geraten ist, nahm an einer Aktuellen Stunde mit Regierungsbefragung und anschließender Fragestunde zum Fall Guttenberg teil. Foto: Wolfgang Kumm dpa/lbn +++(c) dpa - Bildfunk+++ dap 23245789
Kiongozi wa shughuli za chama cha SPD Thomas OppermannPicha: picture-alliance/dpa

Kampeni ya Steinbrueck mwenye umri wa miaka 66 iliikumbana na hali ya kujikwaa wiki iliyopita baada ya kulazimika kujiweka mbali na matamshi yaliyotolewa na mwenyekiti wa chama hicho Sigmar Gabriel aliyetoa wito wa kupunguzwa mwendo kasi katika barabara kuu za Ujerumani hadi kilometa 120 kwa saa.

Waendesha magari wanaona kuwa ni haki yao kuendesha magari katika kasi waitakayo katika mfumo wa barabara kuu nchini Ujerumani. Pamoja na hayo Steinbrueck anapanga kutangaza kile kinachoitwa kikosi cha mapambano chenye wajumbe 10 hadi 12.

Wajumbe watatu katika kikosi chake waliotangazwa leo ni pamoja na afisa wa masuala ya vyama vya wafanyakazi Klaus Wiesehuegel , kiongozi wa wabunge wa SPD bungeni Thomas Oppermann na profesa wa masuala ya ubunifu michoro Gesche Joost ambaye atahusika na sera za chama katika masuala ya Internet.

Mwandishi: Sekione Kitojo /dpae
Mhariri: Yusuf Saumu