1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgogoro wa madeni katika kanda ya Euro

19 Julai 2011

Viongozi wa taifa na serikali wa nchi wanachama wa kanda ya Euro watakutabna alkhamisi ijayo.Lengo ni kusaka njia ya kujikwamua toka janga la madeni ya Ugiriki.

https://p.dw.com/p/11zGo
Kitambulisho cha mgogoro unaozikaba nchi za kanda ya EuroPicha: Fotolia

Mkutano huo umeitishwa na mwenyekiti wa baraza la Umoja wa Ulaya Van Rumpuy.Pembezoni mwa mkutano huo wa viongozi wa taifa na serikali wa nchi wanachama wa kanda ya Euro,mapendekezo kadhaa yamekuwa yakitolewa kuhusu mikakati inayofaa ya kujikwamua.

Katika masoko ya hisa watu wanasubiri vitendo pale viongozi wa taifa na serikali wa nchi wanachama wa zoni ya Euro watakapokutana-kwasababu watabidi waamue hali namna itakavyokuwa.Mapendekezo yapo chungu nzima na kwakua wamebanwa na wakati,kwa hivyo watu wanazungumzia hata masuala miko ambayo hadi wakati huu hakuna aliyeyafikiria.

Kuna wanaofikiria uwezekano kwa Ugiriki na mataifa mengine kununua madeni yao wenyewe lakini kwa bei ya chini kuliko wakati walipokopeshwa.Fedha hizo zitatolewa na mataifa mengine ya kanda ya Europ kupitia fuko maalum la kuinusuru sarafu ya EURO.Faida ya pendekezo hilo ni kwamba mataifa husika yangeweza kushusha pumzi na kuondokana na kitisho cha kukabwa na madeni.

Symbolbild Krise Euro EU Währung Schulden
Sarafu ya Euro na kitambulisho cha Italy,nchi nyengine inayohofiwa isije ikakabwa na madeni kama UgirikiPicha: picture alliance/ZB

Njia hiyo ina hasara pia kwasababu taasisi zinazotathmini uwezo wa serikali kulipa mikopo zitaiangalia njia hiyo kama hatua mojawapo ya kubatilishwa mkopo na wafadhili wa kibinafsi yaani benki na mashirika ya bima kulazimika kufuta mabilioni ya Euro.Pengine anasema Burghard Allgeier wa benki ya kibinafsi ya Hauck und Aufhäuser njia hiyo ikasababisha hasara kubwa kwa Ugiriki.

"Benki za Ugiriki zingefilisika hapo hapo kwasababu akiba zao zisingetosha.Wangezitumia zote."

Matokeo yake yangekuwa kuzusha hali ya mtafaruku katika masoko ya hisa.Mwishoe watu lakini wangepumuwa.Wafadhili mfano wa mkuu wa benki ya biashara ya Ujerumani Commerzbank Martin Blessing anaanza kuzingatia uwezekano kama huo.

Merkel Eurokrise Screenshot der Seite welt.de Flash-Galerie
Kansela Angela Merkel na waziri wake wa fedha Wolfgang SchäublePicha: welt.de

Njia nyengine inayozungumziwa ni kutolewa hisa na nchi wanachama wa kanda ya Euro.Hasara ya njia hiyo ni kwamba Ujerumani kwa mfano ingelazimika kwa mkondo mmoja kulipa asili mia tano kwaajili ya riba kwasababu hapo waatu wangezingatia kiwango cha wastani cha madeni ya pamoja ya nchi za Euro.Mwenyekiti wa benki ya shirikisho Jens Weidmann sawa na wakosoaji wengine wa mpango huo wanahisi mpango huo ungeondowa kiu cha wanaotaka kujiwekea akiba.

Mapendekezo yako mengi na tofauti lakini kama yataweza kutekelezwa haraka hivyo ,kuna wanaotia shaka.

Mwandishi: Ibrahim Samir/Frankfurt(HR)/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Abdul-Rahman,Mohammed