Kiongozi wa Jeshi la Ukombozi wa watu wa kabila la Oromo huko Ethiopia OLA, Jaal Marroo, amesema vikosi vyake vinaukaribia Mji Mkuu Addis Ababa na vinajiandaa kufanya shambulizi. Haya yanafanyika wakati wanadiplomasia wako mbioni kuelekea nchini humo kujadiliana kuhusiana na usitishwaji wa mapigano. Je, mgogoro huu uliodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa unaelekea wapi?