1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Bunge la Marekani laidhinisha azimio la mshikamano na Israel

26 Oktoba 2023

Wabunge wa Marekani wameidhinisha azimio la mshikamano na Israel katika vita vyake dhidi ya Hamas, hii ikiwa ni hatua ya kwanza kuchukuliwa na bunge mara baada ya kupata spika mpya wa Baraza la Wawakilishi, Mike Johnson.

https://p.dw.com/p/4Y2LY
Spika mpya wa bunge nchini Marekani Mike Johnson, ameanza kazi kwa kuongoza kuidhinishwa kwa azimio la mshikamano na Israel
Spika mpya wa bunge nchini Marekani Mike Johnson, ameanza kazi kwa kuongoza kuidhinishwa kwa azimio la mshikamano na IsraelPicha: Stephanie Scarbrough/AP Photo/picture alliance

Hatua hiyo iliyopewa jina "Kusimama na Israel inapojilinda dhidi ya vita vya kikatili vilivyoanzishwa na Hamas na magaidi wengine," ilipata uungwaji mkono wa karibu wabunge wote wa Republican na Democrats. Hata hivyo wabunge 10 wa Democrats hawakupiga kura.

Spika Johnson, mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Republican kutoka Louisiana, katika hotuba yake ya kukubaliwa na bunge alisema jambo la kwanza atakalofanya ni kuwasilisha muswada huo wa kuisaidia Israel.

Johnson, alikuwa ni mgombea wa nne ndani ya mwezi huu kuteuliwa kuwania kiti cha uspika, ambacho kimekuwa wazi tangu tarehe 3 Oktoba baada ya Kevin McCarthy kupinduliwa na wajumbe wa chama chake walioasi.