1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika Kusini

Mfumuko wa bei Afrika Kusini wapungua

24 Mei 2023

Mfumuko wa bei nchini Afrika Kusini kwa mwezi Aprili ulishuka hadi kiwango cha chini kabisa katika takribani mwaka mmoja, ingawa bei za vyakula bado ziko juu.

https://p.dw.com/p/4Rldv
Symbolbild Inflation in Afrika | Simbabwe Lebensmittel
Picha: ZINYANGE AUNTONY/AFP/Getty Images

Hayo yameelezwa leo na shirika la takwimu la serikali, na kwamba mfumuko wa bei wa kila mwaka wa watumiaji ulipungua hadi asilimia 6.8 mwezi uliopita, kutoka asilimia 7.1 mwezi Machi.

Taarifa ya shirika hilo imeeleza kuwa mfumuko wa bei ya vyakula na vinywaji visivyo na kilevi ilirejea kuwa asilimia 13.9 mwezi Aprili kutoka asilimia 14 Machi.

Maziwa, mayai na bidhaa za jibini zilirekodi ongezeko la bei kwa mwaka kwa asilimia 14.5, ongezeko kubwa zaidi tangu Januari, 2009.

Licha ya mfumuko wa bei kushuka kwa jumla, wachambuzi wanatarajia kuwa benki kuu ya Afrika Kusini itaongeza viwango vya riba tena wiki hii.