Mfuko wa uokozi wa euro mashakani
17 Januari 2012Mfuko wa uokozi hauaminiki
Mashirika mengine makubwa ya upangaji viwango , Moody's and Fitch tathmini yao kwa mfuko wa uokozi wa mataifa ya umoja wa sarafu ya euro wenye thamani ya euro bilioni 440 bado ipo katika alama A tatu. Standard and Poor's kinyume chake imepunguza A moja na kuupa mfuko huo wa EFSF A mbili, kwasababu shirika hilo linaziona Ufaransa na Austria , nchi ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa katika mfuko huo, haziaminiki tena kuwa na uwezo wa kukopa katika masoko ya kimataifa.
Mahesabu ni rahisi kabisa , wakati sehemu ya wachangiaji , ambazo ni nchi za umoja wa safaru ya euro zinapungukiwa na uwezo wa kuaminika kukopa, na mfuko huo pia unapoteza uwezo huo. Pamoja na hayo hii haihusiki na kuubana mfuko huo kulipia riba kubwa, ikiwa na maana ya gharama za juu kwa mfuko huo wa EFSF katika kupata michango yake. Kwa hiyo mfuko huo unalitambua hilo.
Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble ameliweka wazi hilo katika mahojiano na radio ya Ujerumani. Mbunge kutoka chama cha CDU katika bunge la Ujerumani Bundestag Michael Meister amesema kuwa ili kuweza kupata tathmini ya juu kutoka kwa mashirika haya na kubakia na alama za juu , ni lazima mataifa husika yaongeze dhamana kwa ajili ya mfuko huo.
Ujerumani haijashushwa
Ujerumani haikushushwa kiwango chake kwa hiyo haipaswi pia kutoa uhakika wa kupatikana kwa euro bilioni 211. Ufaransa na Austria , zimeshushwa na shirika la Standard and Poor's na kupewa alama ya A mbili badala ya tatu. Nchi hizi amesema Meister kuwa zinapaswa kufanya zaidi.
Kwa mtazamo wa waziri wa fedha wa Ujerumani Schäuble hata hivyo anapingana na mawazo hayo na kwamba uhakika wa mfuko huo kuweza kulipa fedha katika muda wa miezi ijayo upo bila shaka.
Hivi sasa imebakia tu Ujerumani kuwa katika hadhi ya juu pamoja na Uholanzi, Finnland na Luxemburg. Inasubiriwa kwa hamu kuona ni masharti gani mfuko huo wa uokozi utatoa leo Jumanne katika kugharamia masoko ya fedha. Rais wa benki kuu ya umoja wa Ulaya Mario Draghi amesema jana katika bunge la ulaya mjini Strassburg kuwa kushushwa huko kuna gharama yake.
Kushushwa kwa hadhi ya mfuko wa EFSF kuna matokeo yake, ambapo iwapo mfuko huo unataka kubakia na hadhi ya alama ya A tatu , inaweza kukopesha kwa kiwango kidogo, ama iwapo haitaweza kubakia na hadhi hiyo bei na gharama za ukopeshaji zitapanda Ama hatua mbadala ni kwamba , ibaki na kiwango chake hicho hicho, iendelee kukopesha kwa uwezo huo huo, bei iwe ile ile, lakini ipate ,michango. Ni lazima kupata michango ya ziada kutoka kwa mataifa yale yenye alama A tatu.
Sarkozy aionya Ulaya
Kutokana na kushushwa kwa hadhi ya kuaminika kwa mfuko wa uokozi katika mataifa ya sarafu ya euro rais wa ufaransa Nicolas Sarkozy ameonya pia kuwa Ulaya inakabiliwa na mzozo mkubwa, na inapaswa kutafuta njia mpya ya kukuza uchumi wake.
Sarkozy ameyasema hayo baada ya mazungumzo yake na waziri mkuu wa Uhispania Rajoy mjini Madrid kuwa sasa mataifa ya ulaya yanapaswa kupunguza matumizi, kupunguza nakisi katika bajeti zao na kutatua matatizo ya ushindani wa ndani.
Mwandishi : Bernd Riegert/ZR/ Sekione Kitojo
Mhariri: Mohammed Khelef
http://www.dw-world.de/dw/article/0,,15669647,00.html