1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Philippe na Malkia Mathilde wa Ubelgiji wawasili DRC

Admin.WagnerD7 Juni 2022

Mfalme Filipo wa Ubelgiji amewasili Kinshasa leo Jumanne akisindikizwa na Malkia Matilda kwa ziara rasmi ya wiki moja nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4CNn4
Belgien | König Philipp empfängt Felix Tshisekedi
Picha: Dirk Waem/AFP/Getty Images

 

 Katika ziara hiyo, mfalme Filipo pamoja na ujumbe muhimu anaouongoza wataenda pia mashariki mwa Kongo, Lubumbashi huko Katanga na Bukavu katika mkoa wa Kivu Kusini.

Wakaazi wa Kinshasa walihamasishwa kujitokeza barabarani ili kuwakaribisha kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa N'djili, Mfalme Filipo na mkewe Malkia Matilda, ambao wanatarajiwa kukutana na viongozi kadhaa wa Kongo ambalo ni koloni la zamani la Ubelgiji.

Serikali za nchi hizi mbili tayari zimekubaliana kuhusu miradi itakayofanywa kuanzia mwaka 2023 hadi mwaka 2027 kwa kiasi cha euro milioni 250 zitakazotolewa na Brussels, kwa mujibu wa Christophe Lutundula, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo.

Soma pia:Tshisekedi akamilisha ziara yake Burundi

"Nguzo ya kwanza ni maendeleo ya uwezo wa vijana, ya pili ni usalama wa chakula kupitia kilimo, tatu ni upatikanaji wa huduma bora za kijamii." Alisema mbele ya ugeni huo akiorodhesha maeneo muhimu ambayo yanaweza kuleta mustakabali wa taifa na ustawi wa jamii.

Aliongeza kwamba utawala shirikishi, mapambano dhidi ya ukatili unaowatendewa wanawake, ushirikishwaji wa wananchi na utawala wa fedha ni maeneo muhimu ambayo serikali ya Kongo inafanyia kazi katika kuboresha maisha ya watu wake.

Ziara hiyo ya kiongozi yakumbusha madai ya Kongo kwa Ubelgiji.

Hapa Kinshasa, Mfalme Filipo na Malkia Matilda wanatarajiwa pia kuzuru Chuo cha Sanaa. Ziara hii inafanyika wakati Ubelgiji inajiandaa kuirejeshea Kongo jino la shujaa wa kitaifa wa Kongo Patrice-Emery Lumumba.

Patrice Lumumba erster Premierminister des unabhängigen Kongo
Patrice Lumumba kiongozi alitazamwa kama mfano wa kuigwaPicha: Everett Collection/picture alliance

Mbali na jino la shujaa wao wakongo wanakumbuka na kudai pia  maelfu ya vyombo vya sanaa vilivyoporwa wakati wa enzi za ukoloni na kuwekwa katika jumba la makumbusho la Tervuren huko Ubelgiji.

Soma pia:Rais Tshisekedi kukutana na viongozi wa waasi wa Kongo

Profesa Henri Bundjoko, Mkurugenzi wa jumba la Makumbusho la Kitaifa  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa upande wake aliikumbusha serikali ya ubelgiji kupanga upya vyombo hivyo zoezi litalosimamiwa na kamati ya wataalamu wa Kongo na Ubelgiji.

"Vitu hivi vitakuja na bila shaka tutavipokea, lakini itabidi tujaribu kuvithibitisha ili kuona ikiwa vitu hivi vinakidhi masharti ya vitu vya zamani"

Alisema Profesa Henri mbele ya serikali ya Ubelgiji, aliongeza kwamba vyombo ambavyo vilibebwa huko Magharibi. Tunapaswa pia kuchunguza kwa umakini.

"kitu kilichochukuliwa wakati wa ukoloni kitakuwa tofauti na kile kilichochukuliwa karne ya ishirini. Hiyo ndiyo kazi ambayo pia tutaifanya." Alisisitiza majukumu ya kamati hiyo ya wataalamu katika kurejesha mali za wakongomani.

Mfalme Filipo na Malkia Matilda kutembelea maeneo muhimu.

Baada ya Kinshasa, Mfalme Filipo na Malkia Matilda pamoja na  ujumbe wao watasafiri Ijumaa hadi mjini Lubumbashi huko Katanga, kabla ya kuelekea  Bukavu mkoani Kivu kusini.

Königin Mathilde König Philippe Belgien
Mfalme Philippe na Malkia Mathilde wa UbelgijiPicha: Aris Messinis/AFP

Hii ni mara ya kwanza Mfalme Filipo kuwasili  Kongo tangu kuchukua ufalme mwaka 2013. Ziara hii  itamalizika Jumatatu wiki ijayo.

Utawala wa kikatili wa Ubelgiji chiniya utawala wa Mfalme Leopold ulianza mwaka 1908 hadi 1960, ambapo mamilioni ya watu waliuawa, kukatwa viungo na kutiwa utumwani.

Soma pia:Wabunge wa Congo wasusia vikao vya bunge

Ubelgiji inatembelea taifa hilo wakati ambapo vikundi vya wapiganaji vimeshamiri kuendeleza mapigano yake Mashariki mwa nchi, huku mamia kwa maelfu ya raia wakiyahama makazi yao.