1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme wa Jordan amteuwa Waziri Mkuu mpya

Angela Mdungu
15 Septemba 2024

Mfalme Abdullah wa Jordan amekubali ombi la kujiuzulu la serikali ya Waziri Mkuu Bisher Khasawneh na amemteua mkuu wake wa utumishi Jafar Hassan kuushika wadhifa huo. Hassan atapaswa kuunda baraza la mawaziri.

https://p.dw.com/p/4ke18
Jordan
Mfalme Abdullah II wa JordanPicha: Hannibal Hanschke/AFP/Getty Images

Waziri Mkuu Khasawneh aliyeingia madarakani Oktoba 2020, aliomba kung'atuka madarakani mapema Jumapili siku chache baada ya uchaguzi wa bunge uliogubikwa na hali ya wasiwasi juu ya vita vya Gaza.

Soma zaidi: Waziri Mkuu wa Jordan Bisher Khasawneh awasilisha ombi la kujiuzulu

Katika uchaguzi huo chama cha upinzani cha Kiislamu cha IAF, ambacho ni tawi la chama cha Udugu wa Kiislamu, kilishinda viti 31 kati ya 138.

Mwaka 1994 Jordan ilitia saini makubaliano ya amani na Israel, lakini imeekuwa na maandamano ya mara kwa mara ya yanayotaka kuvunjwa kwa mkataba huo. Karibu nusu ya raia wa nchi hiyo wana asili ya Palestina.