Katika umri wa miaka 16, mwanariadha Shénidy Tsemane tayari ni bingwa mara mbili wa mchezo wa judo wa Kiafrika katika kitengo cha kilo 57. Matarajio yake makubwa sasa ni kwenda kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwakani nchini Ufaransa na kushinda medali ya dhahabu.