1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meya wa Rio asema maandalizi ya Olimpiki yako

3 Aprili 2015

Meya wa mji wa Rio de Janeiro, Eduardo Paes, amesema kuwa kazi katika mojawapo ya maeneo makuu yatakayotumika kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki 2016 itakayoandaliwa mjini huo itakamilika kwa wakati unaofaa

https://p.dw.com/p/1F2Up
Rio 2016 Maskottchen Olympische Spiele
Picha: picture-alliance/dpa/Alex Ferro

Paes amepuuzilia mbali ripoti kuwa kufutwa kazi kwa wafanyakazi wa ujenzi katika eneo la Deodoro huenda kukachelewesha maandalizi. Meya huyo amesema kufutwa watu kazi kunakofanywa na kampuni ya ujenzi ya Queiroz Galvao ni sehemu ya mkakati usiofaa ili kuishinikiza halmashauri ya mji wa Rio kutoa malipo ya haraka kwa mradi huo utakaogharimu dola za Marekani milioni 205.

Queiroz Galvao ni mojawapo ya makampuni kadhaa ya ujenzi nchini Brazil yanayotuhumiwa kwa kashfa kubwa ya ufisadi katika kampuni ya serikali ya mafuta – Petrobras. "Ukiangalia historia ya Brazil, kila wakati kunatokea matatizo katika kazi za ujenzi, ni kwa sababu kampuni hutishia kusitisha kazi, na kuwafuta wafanyakazi. Hivi ni mbinu za zilizopitwa na wakati. Kwa upande wa Halmashauri ya Rio, nasema kuwa makampuni haya hayatafaulu na mbinu hizi za kutaka fedha zaidi. Yatakamilisha kazi zao kwa wakati ufaao, yatalipwa na yatapata faida yao. Hapatakuwa na ucheleweshwaji wowote wa michezo ya Olimpiki".

Na akizungumza na waandishi wa habari, Paes amesisitiza kuwa shinikizo la kashfa hiyo haliiathiri kazi inayoendelea kwa sasa "Kama kampuni hiyo inawafuta watu kazi, ni haki yake kufanya hivyo, yeyote inayetaka kumfuta. Kama inawaajiri watu wachache, kuwabadilisha wafanyakazi, ni tatizo lao. Kile nisichotaka ni kazi ya ujenzi kusimamishwa. Kama watahitaji watu zaidi wakati wa kipindi Fulani cha kazi, kama wataajiri au la, nnachotaka ni kazi y aujenzi kukamilika".

Eneo la Michezo la Deodoro litaandaa mashindano ya michezo 11 ya Olimpiki ikiwemo ulengaji sabaha, mashindano ya farasi, uendeshaji baiskeli na mambo mengine.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/DPA/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu