1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meya wa Mogadishu afa kwa majeraha ya mashambulizi

2 Agosti 2019

Serikali ya Somalia imetangaza kuwa meya wa mji mkuu, Mogadishu, amefariki dunia baada ya kujeruhiwa vibaya kwenye shambulizi dhidi ya ofisi yake lililofanywa na la kundi la kigaidi la Al-Shabaab wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/3NEHF
Abdirahman Omar Osman | Bürgermeister von Mogadischu nach Anschlag verstorben
Picha: Reuters/F. Omar

Msemaji wa rais wa Somalia amesema Meya Abdirahman Osman alifariki siku ya Alhamisi nchini Qatar alikopolekwa kwa ajili ya matatibu baada ya mashambulizi hayo ya Julai 24.

Kundi la Al-Shabaab na maafisa wa Somalia wamesema mwanamke mshambuliaji wa kujitoa muhanga ndiye alitumika kwenye tukio hilo lililomlenga raia mmoja wa Marekani ambaye ni mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia.

Haijafahamika ni vipi mshambuliaji huyo alifanikiwaje kuingia katika ofisi za meya wakati wageni hulazimika kupita kwenye vizuzi vinne vyenye uwezo wa kutambua mabomu.

Meya Osman aliwahi kuwa diwani mjini London nchini Uingereza kabla ya kurejea Somalia kujiunga na siasa nchini humo.