1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Messi ampiku Ronaldo katika El Classico

24 Aprili 2017

Kinyang'anyiro cha ligi ya Uhispania kimefufuliwa upya baada ya Barcelona kuishinda Real Madrid 3-2 katika mtanange wa El Classico

https://p.dw.com/p/2bomt
Real Madrid vs. Barcelona Lionel Messi
Picha: Reuters/S. Livepic

Lionel Messi alionyesha mchezo safi sana na kuunyamazisha uwanja wa Santiago Bernabeu wakati Muargentina huyo alifunga bao lake la 500 katika klabu ya Barcelona. Nyota huyo alifunga mara mbili na ni bao lake la sekunde ya mwisho ya mchezo lililowanyima Real sare muhimu ya 2-2. Kocha wake Luis Enrique anasema watapambana hadi mwisho "Bila kujali matokeo, kulikuwa na pointi za kutosha za kuweza kushindania. Tuko mbele sasa lakini Real Madrid wana mechi moja ya kucheza hivyo kitakuwa kinyang'anyiro kikali hadi mwisho. Lakini haya ni matokeo ya wazi na ndicho tulichokuwa tukitafuta na tukapata".

Ushindi wa Barca una maana wanatoshana na Real na pointi 75 kileleni mwa La Liga, ijapokuwa Los Blancos wana mechi moja ya kiporo. wa Real Zinedine Zidane amesema kichapo hicho hakimaanishi ndo mwisho wa ligi "Ilikuwa fursa ya kushinda pointi tatu lakini hakutupata, lakini matokeo hayo hayataamua ubingwa. Kama nilivyosema kabla, kushinda, kushindwa, au kutoka sare, haibadilishi chochote lakini ingekuwa vyema kama tungepata hizo pointi tatu. Tunapaswa kukubali kuwa hatukupata na mpinzani wetu akashinda mechi hiyo.

Real sasa wana mechi ngumu ya ugenini dhidi ya Depprtivo la Coruna siku ya Jumatano wakati vinara wa Ligi Barcelona wakipambana na washika mkia Osasuna.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Iddi Ssessanga