1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz:Ulaya ijiandae na uwezekano wa Trump kurejea madarakani

27 Julai 2024

Kiongozi wa upinzani nchini Ujerumani Friedrich Merz amesema Umoja Ulaya unahitaji kujiandaa vyema kwa uwezekano wa Donald Trump kurejea madarakani.

https://p.dw.com/p/4ipDd
Kiongozi wa upinzani nchini Ujerumani Friedrich Merz kutoka chama cha CDU
Kiongozi wa upinzani nchini Ujerumani Friedrich Merz kutoka chama cha CDUPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Merz amesema Ulaya inapaswa kujiandaa licha ya kuwa kwa sasa ushindani ni mkali wa kuwania urais wa Marekani baada ya rais Joe Biden kujiengua na kumuachia nafasi yake Kamala Harris.

Mwanasiasa huyo wa chama cha Christian Democratic Union, CDU ameyasema hayo katika mahojiano yaliyochapishwa leo Jumapili, na kuongeza kuwa Ulaya ilipaswa kufanya hivyo miaka minane iliyopita, akisisitiza kuwa ikiwa atashinda, Trump atakua amejiandaa vilivyo kushikilia wadhifa huo.

Ujerumani pamoja na mataifa mengine ya magharibi ambayo ni washirika wakuu wa Marekani wamekuwa na  hofu ya kurejea kwa Trump madarakani  kutokana na misimamo ya kiongozi huyo hasa kuhusu masuala ya ushirikiano wa kiuchumi na kijeshi.