Merz: Ningekuwa Kansela ningefanya makubaliano na Trump
10 Novemba 2024Matangazo
Akizungumza na jarida la Stern la Ujerumani amesema taifa hilo halina budi kutoka kuwa taifa lililolala lenye uwezo wa kati na kuwa taifa linaloongoza lenye uwezo wa kati.
Kiongozi huyo wa CDU aliituhumu serikali ya Ujerumani kwa namna ilivyojihusisha na uchaguzi wa Marekani ambao Trump alishinda. Amedai kuwa Berlin ilipaswa kuwa tayari kwa matokeo hayo lakini badala yake ilichagua kuwa upande wa mgombea wa Democratic, Kamala Harris.
Merz ndiye anayeonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kumrithi Kansela Olaf Scholz katika uchaguzi wa mapema unaotarajiwa kufanyika mwakani baada ya serikali ya muungano inayoongozwa na Scholz kuvunjika Jumatano.