1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel na Sarkozy wakataa kupunguza kodi ya thamani ya mauzo VAT.

Sekione Kitojo24 Novemba 2008

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Nicolas sarkozy wamekutana mjini Paris leo kuzungumzia uwezekano wa kuibadili hali ya matatizo ya kiuchumi na kifedha duniani.

https://p.dw.com/p/G19M
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akizungumza na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy.Picha: picture-alliance / dpa


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy leo wamekutana mjini Paris kuzungumzia uwezekano wa kuibadili hali ya matatizo ya kifedha na kiuchumi duniani. Mazungumzo hayo yalituwama hususan katika mchango wa kitaifa katika mfuko wa Ulaya wa kuinua uchumi.


Pamoja na mkutano huo wa kansela wa Ujerumani na rais wa Ufaransa, pia wanakutana mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa ya Ulaya pamoja na mawaziri wa mazingira katika mazungumzo kuhusu masuala ya kitaalamu. Na mwishoni kuna mipango wa kuwa na mkutano wa baraza la mawaziri wa Ujerumani na Ufaransa.

Halmashauri ya Ulaya itatoa siku ya Jumatano mapendekezo juu ya mpango wa mageuzi ya kiuchumi, utakaojumuisha Euro bilioni 130. Merkel anataka kuona rasmi baada ya hatua zilizochukuliwa na Ujerumani, kuwa hakuna kitu kitakachotozwa tena kodi.

Ufaransa inaisukuma Ujerumani katika kuwajibika zaidi katika kuuinua uchumi.

Mjini Paris imeelezwa kuwa , Ujerumani ikiwa na uchumi imara katika eneo linalotumia sarafu ya Euro ni lazima ichukue jukumu la kuwa injini ya uchumi wa eneo hilo.

Zaidi ya hayo Ujerumani, kinyume na Ufaransa ambayo ina nakisi kubwa katika bajeti yake , ina nafasi kubwa ya kushughulikia mambo yake.

Viongozi hao wote wawili hata hivyo wanakubaliana juu ya jambo moja nalo ni haja ya dharura duniani kote ya kudhibiti hisa zenye kuleta faida kubwa kwa haraka ambazo pia zina hatari kubwa, pamoja na kuziwekea mbinyo taasisi nyingine za fedha kubadilisha sheria zao katika kuwa na salio la kutosha.

Pia wamejadili kuhusu uwezekano wa kusaidia makampuni ya kuunda magari pamoja na kupitishwa kwa sheria ya mazingira, ili lengo la ulinzi wa mazingira na hatua ya kuinua uchumi liweze kufikiwa kwa pamoja.

Jiwe la msingi la jukwaa la baraza la mawaziri wa Ufaransa na Ujerumani liliwekwa Januari 2003 na rais wa Ufaransa wa wakati huo Jacques Chirac na kansela wa zamani wa Ujerumani Gerhard Schroeder.

Wakati huo huo Ujerumani na Ufaransa zimekubaliana kuwa kupunguza kodi ya thamani ya mauzo sio jibu mjarabu kwa mzozo wa kiuchumi.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amesema baada ya mkutano na kansela wa Ujerumani Angela Merkel leo kuwa iwapo kutakuwa punguzo la VAT , vitu vitapungua bei tu. Amesisitiza kuwa hatua nyingine zimefikiriwa kama kubuni mbinu mpya, na utafiti , zitakuwa hatua bora zaidi kwa ajili ya uchumi.


►◄