1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel na Hollande waadhimisha miaka 50 tangu hotuba ya de Gaulle

Mohamed Dahman22 Septemba 2012

Tarehe 22 mwezi wa Septemba kiongozi mkongwe wa Ufaransa Charles de Gaulle alifunguwa ukurasa mpya katika uhusiano wa Ufaransa na Ujerumani kwa hotuba yenye hamasa.

https://p.dw.com/p/16Cnb
German Chancellor Angela Merkel and French President Francois Hollande meet in front of the castle in Ludwigsburg, Germany, Saturday, Sept.22, 2012. Merkel and Hollande attend the celebration of the 50th anniversary of former French President Charles de Gaulle's speech to the youth of Germany. (Foto:Michael Probst/AP/dapd)
Hollande na MerkelPicha: dapd

Kansela Angela Merkel na mwenzake wa Ufaransa Francois Hollande walihudhuria sherehe hizo katika mji wa kusini magharibi wa Ludwisgsburg Jumamosi (22.09.2012) kuadhimisha miaka 50 tokea kutolewa kwa hotuba mashuhuri kabisa katika historia ya uhusiano wa Ufaransa na Ujerumani. Takriban watu 650 wamehudhuria sherehe hizo.

Maadhimisho hayo yanakumbuka hotuba ya hisia nzito iliotolewa na kiongozi wa kijeshi na wa kisiasa wa Ufaransa Charles de Gaulle kwa lugha ya Kijerumani kwa umati wa vijana wa Kijerumani huko Ludwigsburg hapo mwaka 1962.

Hotuba hiyo inakumbukwa kwa kuwa mwanzo wa uhusiano mpya wa kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani baada ya kumalizika kwa vita na hususan kwamba ujumbe huo umewasilishwa na de Gaulle kiongozi mkali wa Ufaransa aliyeiongoza nchi hiyo wakati wa vita.

German Chancellor Angela Merkel, right, and French President Francois Hollande sit to gather at the castle in Ludwigsburg, Germany, Saturday, Sept.22, 2012. Merkel and Hollande attend the celebration of the 50th anniversary of former French President Charles de Gaulle's speech to the youth of Germany. (Foto:Michael Probst/AP/dapd)
Ludwigsburg 2012Picha: dapd

De Gaulle wakati huo akiwa na umri wa miaka 71 katika hotuba yake ya matumaini aliwapongeza Wajerumani kwa kuwa vijana na kuchambua changamoto mpya ya kizazi kipya kabla ya kuelezea msimamo ambao ulikuwa haufikiriki miaka 20 kabla."Nawapongezeni pia kwa kuwa Wajerumani vijana,ina maana kwamba nyinyi ni watoto wa watu adhimu.

Airbus EADS A320 Montage
Ndege aina ya Airbus A320Picha: dapd

Ndio ni sahihi,watu adhimu! Watu ambao pia wamefanya makosa makubwa katika mkondo wa historia yake." amesema de Gaulle katika hotuba yake hiyo. Kupongezwa huko kwa Wajerumani hususan kulikuwa muhimu kutokana na kutoka kwenye kinywa cha de Gaulle, jenerali pekee mwandamizi kukubali masharti ya Ufaransa ya suluhu ya mwezi wa Juni mwaka 1940 kwa utawala wa Manazi wa Ujerumani katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Ilikuwani miezi michache baadae kufuatia kufuatia hotuba yake hiyo hapo mwezi wa Januari mwaka 1963 ,de Gaulle na Kansela Konrad Adenauer walitia saini Mkataba wa Elysee au Mkataba wa Urafiki ambao ulijenga ushirikiano wa karibu nyanja kadhaa za kisiasa na kiraia.

Mwandishi: Mohamed Dahman. RTR/AFP
Mhariri: Sudi Mnette