Merkel asherehekea miaka 65 ya kuzaliwa
17 Julai 2019Hatarajiwi kwenda umbali huo tena katika maisha yake "Hii ina maana huwezi kuwa kijana tena. Lakini huenda suala la uzoefu zaidi," Merkel amesema wiki iliyopita wakati akiulizwa kuhusu siku yake ya kuzaliwa. Leo ni siku ya kuzaliwa kwa bibi Merkel kuna mengi ya kuzungumzia kuhusu miaka 65 ya maisha yake na kile kinachofuata.
Kansela alizaliwa mnamo Julai 17 , 1954. Amekuwa kansela wa Ujerumani mwaka 2005, kimsingi akifanya mabadiliko makubwa nchini. Mara kadhaa akisifiwa kwa utulivu wake , muda wake madarakani mara nyingi umekuwa na mitikisiko mingi. Waziri wa kilimo Julia Kloeckner alimtakia kansela siku njema ya kuzaliwa kwake kabla ya mkutano wa baraza la mawaziri , akimwita "mtu mwerevu, mwenye busara, mfuasi wa nadharia za vitendo na mwenye uwezo wa kuwa na mwekeleo unaolenga masuala makubwa, huyo ni Angela Merkel.
Anasherehekea siku yake ya kuzaliwa kama ilivyotarajiwa, ameongeza Kloeckner, "bila ya shauku na akifanyakazi."
Merkel ambaye amesema anataka kuendelea kuwa kansela hadi muhula wake utakapomalizika mwaka 2021, hivi karibuni amekuwa akiketi kitini katika shughuli za sherehe za kiserikali. Kutetemeka kulianza kuonekana katikati ya mwezi Juni katika mapokezi ya waziri mkuu mpya wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Kutetema
Merkel alisema wakati huo kuwa alikuwa ameishiwa maji mwilini katika siku ambayo ilikuwa na joto kali. Matukio mengine ya kutetemeka yalielezwa kuwa ni mchakato wa kisaikolojia wa tetemeko la kwanza. Madaktari hawakuwa tayari kuelezea mawazo yao kuhusu afya ya Merkel, ambayo inaelezewa kuwa ni suala la binafsi nchini Ujerumani, hata kama ni kiongozi. Lakini binafsi bibi Merkel leo alisema:
"Najisia vizuri. Nimesema hivi karibuni kuwa nafanyia kazi kile kilichonitokea katika wakati wa gwaride la jeshi na waziri mkuu wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy. Hatua hii bila shaka haijamalizika lakini kuna hatua imepigwa na ninalazimika kuishi na hali hii kwa muda lakini hali yangu ni nzuri na hamna sababu ya kuwa na wasi wasi juu yangu."
Rais wa Urusi Vladimr Putin amempongeza Merkel katika siku yake ya kuzaliwa kwa ujumbe ambao unatoa sifa kwa uongozi wake pamoja na miaka kadhaa ya mafanikio kama kansela.
Merkel ambaye amekuwa kansela tangu mwaka 2005 , ameendelea kuwa kiongozi anayependelewa na watu kwa kiwango cha juu hata pale chama chake cha Christian Democratic Union CDU kimepata kuporomoka katika maoni ya wapiga kura, ambapo inaonesha chama cha walinzi wa mazingira kikionekana kupanda katika umaarufu.