Merkel aelezea imani yake kuhusu sheria ya vinu vya nyuklia
7 Septemba 2010Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema ana amini kuwa sheria yenye utata ya kurefusha muda wa kutumika vinu vya kinyuklia vya nchi hiyo inaweza ikapitishwa bila kuungwa mkono na baraza la wawakilishi wa serikali za majimbo. Kulingana na makubaliano yaliyofikiwa siku ya Jumapili, vinu hivyo 17 vitaendelea kutumika kwa muda wa wastani miaka 12.
Serikali hiyo ya Muungano ya Ujerumani pia ilikubaliana kuhusu kodi ya Euro bilioni 2.3 kwa mwaka kutokana na faida za makampuni ya nishati. Mwaka 2000, serikali ya kansela wa zamani wa Ujerumani, Gerhard Schroeder iliamua kuvifunga vinu vyote vya nyuklia ifikapo mwaka 2021.
Bibi Merkel anataka kuongeza muda huo kama hatua ya kuziba pengo hadi hapo vyanzo vya nishati mbadala vitakapokuwa bora zaidi. Vyama vya upinzani na wana mazingira wameahidi kupinga uamuzi huo wakati ambapo unapelekwa kujadiliwa bungeni.