Kuhusu mambo yanayoendelea kati ya Tanzania na nchi jirani za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC, katika harakati za kukabiliana na janga la virusi vya corona DW ilitaka kufahamu zaidi uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na nchi jirani umesimama wapi. Grace Kabogo amezungumza na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Tanzania, Bernard Membe.