1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meli ya msaada wa Gaza yaanza safari kuelekea huko

13 Machi 2024

Meli ya misaada ya Uhispania inayopeleka chakula katika eneo la Gaza imeondoka Cyprus Jumanne ikwa safari ya mwanzo ya kupeleka misaada inayohitajika sana katika eneo lililoharibiwa na vita la Palestina.

https://p.dw.com/p/4dRqT
Meli ya Open Arms iliyobeba msaada wa chakula cha kibinadamu katika bandari ya Cyprus ya Larnaca
Meli ya misaada ya Uhispania ikiwa na tani 200 za msaada wa chakula kwa ajili ya Gaza iliyoharibiwa na vita ilisafiri kutoka kisiwa cha Cyprus, Machi 12.Picha: AFP

Meli hiyo inayoitwa "The Open Arms" iling'oa nanga kutoka bandari ya Larnaca kwenye bahari ya Mediterania, ikiwa imesheheni tani 200 za bidhaa za msaada kwa ajili ya safari ya baharini ya takriban kilomita 400,

Kama ishara ya kuzorota kwa hali ya kibinadamu kwa zaidi ya miezi mitano tangu vita hivyo kuzuka, wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza unaotawaliwa na Hamas imesema "idadi ya vifo kutokana na utapiamlo na upungufu wa maji mwilini iliongezeka hadi 27", wengi wao wakiwa watoto.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen aliita kuondoka kuwa "ishara ya matumaini", na kuonesha niakuongeza jitihada ya meli nyingi za misaada kufika katika eneo hilo.