1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meli mbili zashambuliwa nje ya eneo la Wahouthi

Josephat Charo
3 Septemba 2024

Meli mbili za biashara zimeshambuliwa na waasi wa Houthi nje ya pwani ya mkoa wa Hodeida nchini Yemen. Waasi wa Houthi wamedai wamehusika na mashambulizi dhidi ya meli hizo.

https://p.dw.com/p/4kCYZ
Waasi wa Houthi wamekuwa wakizishambulia meli katika bahari ya Shamu
Waasi wa Houthi wamekuwa wakizishambulia meli katika bahari ya ShamuPicha: David Mackinnon/AP/picture alliance

Vyombo vya usalama wa baharini vimesema meli mbili za kibiashara zimeshambuliwa nje ya pwani ya mkoa wa Yemen unaodhibitiwa na waasi wa Hodeida. Vyombo hivyo pia vimesema wafanyakazi wote katika meli hizo wako salama.

Kituo cha pamoja cha kutoa taarifa za safari za baharini kimesema meli ya kwanza iliyotambuliwa kama Blue Lagoon ya Panama, ililengwa na makombora mawili ya masafa marefu, huku kombora la tatu likiyapiga maji kiasi mita 50 kutoka kwa meli hiyo.

Waasi wa Houthi wamesema katika taarifa wameishambulia meli hiyo kwa makombora na droni na ililengwa moja kwa moja.

Meli hiyo haikuharibika sana na haihitaji msaada wowote na inaendelea na safari yake kuelekea bandari iliyopangiwa.

Katika tukio lengine jana Jumatatu meli nyingine ya kibiashara ilishambuliwa kutumia droni magharibi mwa Hodeida, lakini hakuna uharibifu wowote wala maafa yaliyotokea.