1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MEKKA: Hamas na Fatah wakubali kugawana wizara

8 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTt

Makundi hasimu ya Wapalestina,Hamas na Fatah, yamekubaliana kuhusu ugawaji wa nyadhifa za wizara katika serikali ya umoja wa taifa. Maendeleo hayo yamepatikana siku ya pili ya majadiliano yanayofanywa mji takatifu wa Mekka nchini Saudi Arabia.Pande hizo mbili ziliahidi kuwa hazitoondoka bila ya kuafikiana.Kuambatana na makubaliano hayo mapya,chama tawala cha Hamas kitapewa nyadhifa saba wakati Fatah cha rais Mahmoud Abbas kitakuwa na sita.Wizara muhimu ya mambo ya ndani inayodhibiti vikosi vya usalama, itakwenda kwa mtaalamu huru atakaechaguliwa na Hamas.Kwa upande mwingine,chama cha Fatah kitamchagua mtaalamu alie huru,kuongoza wizara ya mambo ya nje.