1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MECCA : Waislamu waanza Hija kwa amani

29 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfP

Serikali ya Saudi Arabia inasema hija ya mwaka huu inaendelea kufanyika kwa amani kwa mujibu ilivyopangwa.

Takriban Waislamu milioni tatu wako katika mji mtakatifu wa Mecca kuanza hija hiyo ya siku tano kujitakasa na dhambi. Hija ya mwaka huu inafanyika wakati kukiwa na hali ya mvutano kati ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni na Washia lakini serikali ya Saudi Arabia imeonya kwamba itavunjilia mbali jaribio lolote lile la kudhoofisha usalama wakati wa kipindi hiki cha hija.

Maelfu ya askari wa usalama wa Saudi Arabia wamemwagwa kwenye njia za kupitia mahujaji wakati wa kutekeleza ibada hiyo pamoja na kuwekwa kwa madarzeni ya vituo vya afya kwenye maeneo yote husika.

Mwaka jana watu 364 walipoteza maisha yao kutokana na mkanyagano na hapo mwaka 2004 zaidi ya watu 250 walikufa kutokana na mkanyagano.

Ibada ya Hija ni nguzo ya tano ya Kiislam ambapo inamwajibikia kila mwenye uwezo na afya kuitekeleza angalau mara moja katika kipindi cha uhai wake.