1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mda wa majeshi ya nje kubaki Afghanistan warefushwa

21 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DSIj

NEW YORK:

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kuongeza mda wake nchini Afghanistan.Baraza la wanachama 15 limepitisha kwa kauli moja,pendekezo la kuimarisha uungaji mkono wa serikali ya Afghanistan,kuboresha juhudi za ukarabati na pia uratibu wa mipango ya usalama ya nchi hiyo. Hatua ya baraza hilo inarefusha uhalali wa kuwepo huko majeshi ya kigeni kwa mda mwingine wa mwaka mmoja.Balozi wa afghanistan katika Umoja wa Mataifa,Zahir Tanin, amesema kuwa ujumbe wa kura ya Umoja wa Mataifa,unaonyesha kama jamii ya kimataifa inanuia kubaki nchini Afghanistan licha ya matatizo ya kiusalama.Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amekaribisha uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa,akisema ni ishara nzuri ambayo imekuja kwa wakati muafaka.