1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mchuano ni mkali katika kura ya mabadiliko Venezuela

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVtG

CARACAS.Matokeo ya Kura ya mabadiliko ya katiba nchini Venezuela yanaonesha kuwa mvutano ni mkubwa kati ya wanaounga mkono na wasiyounga mkono.

Kura hiyo ilipigwa jana juu ya mabadiliko yaliyopendekezwa na Rais Hugo Chavez ambayo ni pamoja na kutokuwepo kwa ukomo wa kugombea urais na kusitisha uhuru wa Benki Kuu ya nchi hiyo.

Makamu wa Rais wa Venezuela Jorge Rodriguez ambaye aliongoza kampeni za Rais Chavez amesema kuwa hali ni ya mvutano mkali.

Mapema Rais Chavez wakati akipiga kura alisema kuwa ana matumaini ya kuungwa mkono lakini akasema pia kuwa atakubaliana na matokeo yoyote yatakayotangazwa.

Akiyatetea mababdiliko hayo kiongozi huyo mwenye mrengo wa kisoshalisti amesema kuwa yataupa umma madaraka zaidi.

Wapinzani wamekuwa wakifanya mikutano kadhaa kupinga mabadiliko hayo wakisema kuwa Rais Chavez ana nia ya kung´ang´ania madaraka.

Watu wengi walijitokeza kupinga, ambapo katika mji mkuu Caracas kulikuwa na mistaari mirefu ya wapiga kura.