Brazil imeanza siku tatu za maombolezo ya kitaifa ya nguli wa kandanda nchini humo Pele. Mshindi huyo mara tatu wa Kombe la Dunia anazingatiwa na wengi kuwa mchezaji bora kabisa wa muda wote. Miongoni mwa waliobahatika kumuona na pia kucheza naye ni mwanasoka nguli nchini Tanzania Sunday Ramadhan Manara. Anamzungumziaje Pele? Sikiliza mahojiano yake na Bruce Amani.